Kuna siku nilichalala kipesa nikaamua kuomba dem wangu aniazime 10,000/= akanipa. Baada ya siku mbili nikapata pesa zaidi ya laki nne hivi, nikaamua kumpa 100,000/= mpenzi wangu bila yeye kuniomba. Baada ya siku 3 akaja kuniambia:- “Bae, ile 10,000/- niliyokuazima mwenyewe amekuja kunidai, so kama unayo naomba unipe nimrudishie maana ananisumbua leo siku ya 3.” SAA HIZI NIPO ZANGU SINGLE NATAFUTA DEM MWINGIN
Tukiwa kanisani mdada alikuwa amelala , akaamka akasikia Pastor anasema ” SIMAMA” Yule dada akasimama akashangaaa kanisa zima linamtizima kwa mshangao akiwemo mumewe, akaangalia kanisa zima akashtuka kujiona yeye peke yake ndiye aliesimama Pastor akaendelea vizur endelea kusimama, tumepata mmoja hadi sasa aliyesimama narudia kwa mara ya mwisho kama hujasikia vizuri ” kama wew umewahi kumsaliti au bado unasaliti ndoa yako SIMAMA” Binti akazimia
Comments
Post a Comment